50 Cent alivyokuwa zamani kushoto na alivyo sasa kulia.(picha baadaye)50 Cent amejikondesha kwa kunywa maji na juice pekee ili aweze kuigiza kwenye filamu mpya ambayo jikoni ambayo inamuelezea nyota wa mpira wa miguu ambaye anaugua ugonjwa wa kansa.
50 Cent ambaye ana umri wa miaka 34 amekonda sana na amepungua uzito wake toka kilo 97 hadi kilo 72.
50 Cent amejikondesha ili kuleta uhalisia wa mgonjwa wa kansa katika filamu ya "Things Fall Apart", filamu hiyo 50 Cent ndiye nyota wa filamu na prodyuza msaidizi.
Wakati picha mpya za 50 Cent zilipowekwa kwenye mitandao jana watu wengi waligoma kuamini na kusema kwamba picha hizo ni uzushi tu wa kwenye mitandao.
Lakini 50 Cent ambaye jina lake halisi ni Curtis Jackson alijitokeza na kuthibitisha kuwa picha hizo ni za kweli.
50 Cent alisema kuwa baada ya kumaliza kuigiza kwenye filamu hiyo ataanza kula kama kawaida kurudisha mwili wake wa zamani.
Thursday, June 3, 2010
Bibi wa China Aota Mapembe Kama Mbuzi
Bibi Zhang Ruifang mwenye umri wa miaka 101 wa kijiji cha Linlou katika jimbo la Henan nchini China alianza kuota pembe moja kwenye kichwa chake mwaka jana. Hadi sasa pembe hilo lililoota kwenye upande wa kushoto wa paji lake la uso limekua na kufikia urefu wa sentimeta sita. Upande wa kulia wa paji lake la uso kuna pembe jingine ambalo ndio kwanza linaanza kujitokeza. Familia yake imepagawa na mapembe hayo na haijui kwanini yanajitokeza kwenye kichwa chake. Mtoto wa mwisho wa bibi huyo anayeitwa Zhang Guozheng mwenye umri wa miaka 60 alisema kuwa wakati mapembe hayo yalipoanza kujitokeza mwaka jana hawakujali sana walidhania ni makunjamano ya ngozi tu. "Lakini siku zilivyozidi kwenda pembe lilijitokeza kwenye kichwa chake na sasa limefikia sentimita sita" alisema Zhang ambaye kaka yao wa kwanza ana umri wa miaka 82. "Hivi sasa kuna kitu kinajitokeza kwenye upande wa kulia wa paji lake la uso bila shaka ni pembe jingine", aliendelea kusema Zhang. Madaktari walisema kuwa mapembe hayo yanaweza kuondolewa kwa operesheni lakini sababu ya kujitokeza kwa mapembe hayo bado haijulikani. | ||
| ||
|
Subscribe to:
Posts (Atom)