Tuesday, June 1, 2010
Mtoto wa Miaka Miwili Anayevuta Sigara 40 Kwa Siku
Ardi Rizal mtoto mwenye umri wa miaka miwili ambaye amekuwa akivuta sigara 40 kwa siku amekuwa gumzo duniani baada ya video kutolewa ikumuonyesha mtoto huyo jinsi anavyovuta sigara kwa wingi huku akicheza na watoto wenzake.
Ardi alianza kuvuta sigara akiwa na umri wa miezi 18 lakini hivi sasa akiwa na umri wa miaka miwili wazazi wake wanalalamika kuwa amekuwa mvutaji sigara sugu kiasi cha kufanya vurugu kubwa sana anaponyimwa sigara.
"Ardi anaponyimwa sigara huwa mwenye hasira sana na hufanya vurugu na wakati mwingine hujibamiza kichwa chake ukutani", alisema mama yake Diana mwenye umri wa miaka 26.
Kutokana na unene wake na jinsi anavyovuta sigara kwa fujo, Ardi anashindwa kukimbizana na watoto wenzake.
Serikali ya Indonesia iliahidi kuipa familia ya Ardi zawadi ya gari jipya iwapo Ardi ataacha kuvuta sigara. Lakini jitihada zote za kumuachisha Ardi sigara zimegonga mwamba na badala yake Ardi huifanya familia yake itumie takribani Tsh. 8,000 kila siku kwaajili ya kumnunulia sigara.
Baba yake ambaye anafanya kazi ya kuuza samaki, haoni hatari inayomkabili mtoto wake na husema kwamba mtoto wake ana afya njema hana matatizo yoyote.
"Sina wasiwasi wowote kuhusiana na afya yake, Ardi ni mtoto mwenye afya njema", alisema baba yake kuwaambia waandishi wa habari.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment