Wednesday, May 19, 2010

Matiti Yenye Uzito wa Kilo 12 Yamlaza Kitandani


Julia Manihuari [29] mama wa watoto wanne wa nchini Peru alisumbuliwa na ugonjwa wa ajabu ambao uliyafanya matiti yake yawe makubwa sana na kufikia ukubwa wa saizi N.

Matiti yake yalikuwa na uzito wa kilo 12 hali iliyomfanya ashindwe kuendelea na shughuli zake za kila siku na kutumia muda mwingi kitandani.

Julia alianza kuona mabadiliko kwenye matiti yake baada ya kujifungua mtoto wake wa tatu miaka saba iliyopita. Matiti yake yalizidi kuwa makubwa siku hadi siku.

Alipojifungua mtoto wa nne, matiti yake yalizidi kuwa makubwa zaidi, titi la kushoto lilikuwa na uzito wa kilo tano wakati la kulia lilikuwa na uzito wa kilo saba.

Wakati alipokuwa akisimama matiti yake yalikuwa yakimzidia uzito na alipokuwa akilala uzito wa matiti yake kifuani ulimfanya apumue kwa tabu.

Kwa miaka kadhaa Julia aliendelea kuteseka na hali hiyo kwakuwa yeye na mumewe ni wakulima maskini na hawakuwa na uwezo wa kulipia gharama za matibabu.

Julia hatimaye alifanikiwa kupata tiba mwaka huu baada ya wafadhili kujitokeza baada ya habari kuhusiana na mateso yake zilipotolewa kwenye magazeti.

Madaktari nchini Peru walifanikiwa kuyafanyia operesheni matiti yake na kuyapunguza kufikia ukubwa wa saizi B.

Julia hivi anaishi maisha ya furaha baada ya kuondokewa na uzito wa matiti yake uliomtesa kwa miaka mingi sana.


No comments: